Monday to Friday: 8 AM - 5 PM
Mkwakwani, Tanga
cropped-LOGO-MAKAZI.png
Email Us
info@makazisolutions.com
Call Us
+255 703146147
Get Started
Kipumbwi
City ProjectKipumbwi Satelite City
Kipumbwi Satellite City — Pangani

HAKIKA KIPUMBWI SATELLITE CITY NI KIUNGO MUHIMU KATIKA KUBORESHA BIASHARA YA UTALII NCHINI 

Ni Mradi wa kimkakati unaounganisha Tanga kwa kilometa 80, Dar es Salaam kwa kilomita 180 na kilomita 60 tu hadi Zanzibar. Viwanja vimepakana na barabara mpya ya Lami ya Tanga-Pangani-Kipumbwi-Bagamoyo mpaka Dar es Salaam. Ambapo kukamilika kwa barabara hiyo  itapunguza safari ya Tanga-Dar es Salaam kwa takribani kilometa 90. 

Hii itapelekea idadi kubwa ya magari kuhama toka barabara ya Segera. Pia viwanja vipo  km 3 tu toka Bandari ya Kipumbwi ambapo kunajengwa soko la Samaki na kiwanda cha kukaushia dagaa cha shilingi bil. 1.3.Hivyo vinaufanya Mji wa Kipumbwi kukua haraka na kuwa kitovu kipya cha uchumi wa buluu, biashara, usafirishaji, uvuvi, bandari na watalii wanaotoka Zanzibar, Mbuga ya Saadan na Kisiwa cha Maziwe.

Aidha mradi huu Kupitia vivutio vilivyosahaulika Mkoani Tanga{Magofu ya Tongoni na Pangani, Makaburi ya vita ya kwanza ya dunia Usagara, shule ya Kwanza ya Mkoloni Magila na Safu ya Milma ya Luhoto na Amani} unaunganisha watalii  na uwanda mkuu wa vivutio vya Utalii Kaskazini{Mlima Kilanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Manyara na venginevyo vingi}.

WhatsApp Image 2026-04-30 at 1.09.58 PM (1)
Take Action Now
Get in Touch Today
Experience our tailored services designed for effective land transformation and development.
Contact Us Now

UTARATIBU WA KUPATA VIWANJA

1.    Mteja atachagua kiwanja kupitia ramani atakayopatiwa na kampuni.

2.    Mteja atafanya booking kwa kujaziwa fomu kwa gharama ya shilingi 20,000.{malipo ya awali yafanyike ndani ya siku 7 kinyume chake kiwanja kitaacha huru kwa mteja mwingine}

3.    Mteja anaruhusiwa kufika site au kutuma mwakilishi kuhakiki eneo lake alilolichagua {ndani ya muda wa booking}

4.    Mteja ana nafasi ya kubadilisha kiwanja iwapo hatoridhika na eneo alichochagua na kulilipia kabla ya kufika site.

5.    Malipo yote yatafanyika kupitia akaunti ya Kampuni

6.    Baada ya kufika site kwa gharama za mteja huduma ya kutembelea na kuonyeshwa maeneo Kipumbwi inatolewa kila siku na muda wote na Kampuni

7.   Mteja atatakiwa kuwasilisha nyaraka za uthibitisho wa malipo ya banki na kupewa risiti ya kampuni.

8.    Iwapo mteja atalimbikiza malipo ya miezi miwili na kuendelea pasipo kutoa taarifa na kuidhinishwa na kampuni mteja atapoteza sifa yakuendelea kubaki na kiwanja hicho na kitapatiwa mteja mwingine.

9.    Ikiwa mteja atashindwa kuendelea na malipo anatakiwa kutoa taarifa kwa kampuni ili kiwanja chake kiuzwe kwa mteja mwingine na pesa itarejeshwa baada ya miezi 8 na itakatwa asilimia 20 ya usumbufu.

10.    Baada ya kukamilisa malipo mteja atajaza fomu namba 19 ya maombi ya kumiliki ardhi sambamba na fomu ya kampuni yakuthibitisha kukamilisha malipo na atawasilisha nakala ya nida Pamoja na picha mbili kwa kila kiwanja.

11.    Kampuni itamsaidia mteja kufungua akaunti ya maombi ya kumiliki ardhi{E-ardhi} Pamoja na ufuatiliaji wa hati miliki.

12.   Mteja atawajibika kulipia kodi ya ardhi na gharama nyingine za maandalizi ya hati kwa serikali

Marine Commercial Zone

- Uvuvi (Samaki na Dagaa)

- Zana za Uvuvi

- Matengenezo ya Boti na Vifaa (Boat Yard)

Business Hub

- Ujenzi wa soko la samaki na dagaa

- Uwepo wa wahitaji kutoka nje ya nchi

- Uwepo wa Bandari ya Kipumbwi

- Ukaribu na Zanzibar kwa Km 60

- Ukaribu na Dar Es Salaam kwa Km 180

- Usafirishaji wa Bidhaa kutoka na kwenda Zanzibar

Fursa ya Utalii

- Ukaribu na Mbuga ya Saadani National Park

- Beach Plots za Hotels 

- Ukaribu na Kisiwa cha Maziwe

All logos belong to their respective owners