Monday to Friday: 8 AM - 5 PM
Mkwakwani, Tanga
cropped-LOGO-MAKAZI.png
Email Us
info@makazisolutions.com
Call Us
+255 703146147
Get Started
Kilapula Project 
Makazi Solutions LtdKilapula Azimio Project
Kilapula Azimio Ngomeni Project

Mradi wa kwanza uliopo kilomita 20 tu toka Tanga Mjini na kilomita 2 toka Mizani ya Pongwe. Eneo linapakana na barabara ya lami ya Tanga–Segera, bomba la mafuta EACOP na reli ya kati inayobadilishwa kuwa ya kisasa (SGR)  na stesheni ya Ngomeni iliyopo ndani ya mradi huo.

Huduma za kijamii kama umeme, maji, vituo vya afya, shule zinapatikana

Hii itapelekea idadi kubwa ya magari kuhama toka barabara ya Segera. Pia viwanja vipo km 3 tu toka Bandari ya Kipumbwi ambapo kunajengwa soko la Samaki na
kiwanda cha kukaushia dagaa cha shilingi bil. 1.3.Hivyo vinaufanya Mji wa
Kipumbwi kukua haraka na kuwa kitovu kipya cha uchumi wa buluu, biashara, usafirishaji, uvuvi, bandari na watalii wanaotoka Zanzibar, Mbuga ya Saadan na Kisiwa cha Maziwe.

Aidha mradi huu Kupitia vivutio vilivyosahaulika
Mkoani Tanga{Magofu ya Tongoni na Pangani, Makaburi ya vita ya kwanza ya dunia
Usagara, shule ya Kwanza ya Mkoloni Magila na Safu ya Milma ya Luhoto na Amani}
unaunganisha watalii  na uwanda mkuu wa
vivutio vya Utalii Kaskazini{Mlima Kilanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Manyara na
venginevyo vingi}.

KILAPULA MAP.jpg
Take Action Now
Get in Touch Today
Experience our tailored services designed for effective land transformation and development.
Contact Us Now

UTARATIBU WA KUPATA VIWANJA

1.    Mteja atachagua kiwanja kupitia ramani atakayopatiwa na kampuni.

2.   Mteja atafanya booking kwa kujaziwa fomu kwa gharama ya shilingi 20,000.{malipo ya awali yafanyike ndani ya siku 7 kinyume chake kiwanja kitaacha huru kwa mteja
mwingine}

3.   Mteja anaruhusiwa kufika site au kutuma mwakilishi kuhakiki eneo lake alilolichagua {ndani ya muda wa booking

4.   Mteja ana nafasi ya kubadilisha kiwanja iwapo hatoridhika na eneo alichochagua na kulilipia kabla ya kufika site

5.   Malipo yote yatafanyika kupitia akaunti ya Kampuni

6.    Baada ya kufika site kwa gharama za mteja huduma ya kutembelea na kuonyeshwa maeneo Kipumbwi inatolewa kila siku na muda wote na Kampuni

7.   Mteja atatakiwa kuwasilisha nyaraka za uthibitisho wa malipo ya banki na kupewa
risiti ya kampuni.

8.   Iwapo mteja atalimbikiza malipo ya miezi miwili na kuendelea pasipo kutoa taarifa na kuidhinishwa na kampuni mteja atapoteza sifa yakuendelea kubaki na kiwanja
hicho na kitapatiwa mteja mwingine.

9.   Ikiwa mteja atashindwa kuendelea na malipo anatakiwa kutoa taarifa kwa kampuni ili kiwanja chake kiuzwe kwa mteja mwingine na pesa itarejeshwa baada ya miezi 8 na
itakatwa asilimia 20 ya usumbufu.

10.   Baada ya kukamilisa malipo mteja atajaza fomu namba 19 ya maombi ya kumiliki ardhi sambamba na fomu ya kampuni yakuthibitisha kukamilisha malipo na atawasilisha nakala ya nida Pamoja na picha mbili kwa kila kiwanja.

11.    Kampuni itamsaidia mteja kufungua akaunti ya maombi ya kumiliki ardhi{E-ardhi} Pamoja na ufuatiliaji wa hati miliki.

12.   Mteja atawajibika kulipia kodi ya ardhi na gharama nyingine za maandalizi ya hati kwa serikali

KILAPULA MAP.jpg
All logos belong to their respective owners