Mradi Unaendelea
Kipumbwi Satellite City
Kipumbwi Satellite City ni mradi wa jiji jipya lililopangwa na kupimwa rasmi huko Pangani, Tanga. Mradi una jumla ya viwanja 4,073 kwa matumizi ya makazi, biashara na matumizi mchanganyiko, ukiwa na mpangilio wa barabara na maeneo ya huduma mbalimbali.
Muhtasari wa Mradi
Kipumbwi Satellite City
Kipumbwi Satellite City ni mradi wa jiji jipya lililopangwa na kupimwa rasmi huko Pangani, Tanga. Mradi una jumla ya viwanja 4,073 kwa matumizi ya makazi, biashara na matumizi mchanganyiko, ukiwa na mpangilio wa barabara na maeneo ya huduma mbalimbali.
Makazi Solutions (T) Limited inatekeleza huduma za upangaji miji, uendelezaji wa ardhi, upimaji na huduma nyingine zinazohusiana na matumizi na umiliki wa ardhi kwa kuzingatia taratibu za kitaalamu.
Fursa za Uwekezaji
Fursa za Uwekezaji Katika Mradi wa Kipumbwi Satellite City
Ramani na Umbali
Iko Wapi na Utafikaje?
Kipumbwi Satellite City iko Wilaya ya Pangani, Mkoa wa Tanga, kando ya Bahari ya Hindi. Barabara mpya ya lami ya Dar – Bagamoyo – Pangani – Tanga (km 260) inapita Kipumbwi, na inapunguza safari kwa km 90 ukilinganisha na njia ya Segera (km 350).
Ramani za Mradi
Ramani za Mradi wa Kipumbwi Satellite City
Tazama Video
Fursa za Uwekezaji Kipumbwi, Tanga
Tazama eneo la Kipumbwi Satellite City na fursa zake za makazi, biashara na uwekezaji katika ukanda wa pwani wa Pangani, Tanga.
Maswali ya Mara kwa Mara
Una Swali? Haya Ndiyo Majibu
Kiwanja cha Kipumbwi Satellite City kinaanzia bei gani?+
Viwanja vinapatikana kwa bajeti kuanzia Tsh 3,000,000. Bei halisi inategemea ukubwa, matumizi (makazi, biashara au mchanganyiko) na eneo la kiwanja ndani ya mradi.
Booking ni kiasi gani na inafanya nini?+
Booking ni Tsh 20,000. Inahifadhi kiwanja ulichochagua wakati unakamilisha taratibu za malipo na umiliki.
Nalipaje kiwanja?+
Baada ya kuchagua kiwanja, unalipa asilimia 50 ya bei kama malipo ya awali. Kiasi kinachobaki hulipwa kwa awamu, kulingana na masharti ya mauzo.
Naweza kununua kwa mkopo wa benki?+
Ndiyo. Makazi Solutions ina ushirikiano na Benki ya TCB unaowezesha kumiliki kiwanja kilichopimwa kwa malipo ya awamu. Wasiliana nasi au tembelea tawi la TCB kwa masharti kamili.
Je, viwanja vimepimwa rasmi?+
Ndiyo. Viwanja vya Kipumbwi Satellite City vimepangwa na kupimwa rasmi na wataalamu waliosajiliwa wa upangaji miji na upimaji ardhi.
Nitapata hati ya umiliki?+
Makazi Solutions inasaidia maandalizi na mchakato wa hati za umiliki, ikiwemo Certificate of Right of Occupancy (CRO) na Certificate of Customary Right of Occupancy (CCRO), kulingana na aina ya umiliki wa ardhi.
Je, napewa risiti ya malipo?+
Ndiyo. Kila malipo yanapaswa kuwa na risiti rasmi ya kampuni. Usilipe bila kupokea risiti.
Naweza kutembelea eneo kabla ya kununua?+
Ndiyo, na tunashauri ufanye hivyo. Panga site visit kwa kutupigia simu au kutuandikia WhatsApp 0790 398 189.
Mradi uko wapi hasa?+
Kipumbwi, Wilaya ya Pangani, Mkoa wa Tanga, kando ya Bahari ya Hindi, takribani kilomita 1.5 kutoka Bandari ya Kipumbwi.
Umevutiwa na Kipumbwi Satellite City?
Wasiliana na Makazi Solutions kupata taarifa zaidi kuhusu mradi, viwanja vinavyopatikana, bei na taratibu za umiliki.




