Kipumbwi Satellite City
Weka Booking ya Kiwanja
Jaza fomu ya hatua 4 hapa chini na uchague afisa wa kukuhudumia. Atawasiliana nawe kuhusu kiwanja, bei na hatua za umiliki.
Hatua za Booking
Jinsi ya Kuweka Booking
01 · Chagua Kiwanja
Chagua bajeti na matumizi ya kiwanja kinachokufaa.
02 · Weka Booking
Jaza fomu, chagua afisa wako na tuma taarifa zako.
03 · Lipa Asilimia 50
Kamilisha malipo ya awali baada ya kuthibitisha kiwanja.
04 · Saini Mkataba
Kamilisha nyaraka, kisha tunaratibu Hati Miliki yako.
Weka Booking
Chagua Kiwanja na Uweke Booking
Hatua 4 tu: jaza taarifa zako, chagua bajeti na matumizi, chagua afisa wako, kisha tuma kwa WhatsApp, Email au Simu.
Lipa kwa Awamu
Ushirikiano wa Makazi Solutions na Benki ya TCB
Sasa unaweza kumiliki kiwanja kilichopimwa kwa kulipa kwa awamu kupitia Benki ya TCB. Tazama video kufahamu zaidi kuhusu makubaliano haya, kisha wasiliana nasi au tembelea tawi la TCB lililo karibu nawe kwa maelezo ya masharti.
Hati Miliki
Tunakusaidia Kupata Hati Miliki
Kampuni ya Makazi Solutions inamsaidia mteja kuratibu mchakato wa upatikanaji wa Hati Miliki ya kiwanja chake, ili kuhakikisha anapata umiliki rasmi wa kisheria wa ardhi.
Gharama za upatikanaji wa Hati Miliki hazijajumuishwa kwenye bei ya kiwanja.

Maswali ya Mara kwa Mara
Una Swali? Haya Ndiyo Majibu
Kiwanja cha Kipumbwi Satellite City kinaanzia bei gani?+
Viwanja vinapatikana kwa bajeti kuanzia Tsh 3,000,000. Bei halisi inategemea ukubwa, matumizi (makazi, biashara au mchanganyiko) na eneo la kiwanja ndani ya mradi.
Booking ni kiasi gani na inafanya nini?+
Booking ni Tsh 20,000. Inahifadhi kiwanja ulichochagua wakati unakamilisha taratibu za malipo na umiliki.
Nalipaje kiwanja?+
Baada ya kuchagua kiwanja, unalipa asilimia 50 ya bei kama malipo ya awali. Kiasi kinachobaki hulipwa kwa awamu, kulingana na masharti ya mauzo.
Naweza kununua kwa mkopo wa benki?+
Ndiyo. Makazi Solutions ina ushirikiano na Benki ya TCB unaowezesha kumiliki kiwanja kilichopimwa kwa malipo ya awamu. Wasiliana nasi au tembelea tawi la TCB kwa masharti kamili.
Je, viwanja vimepimwa rasmi?+
Ndiyo. Viwanja vya Kipumbwi Satellite City vimepangwa na kupimwa rasmi na wataalamu waliosajiliwa wa upangaji miji na upimaji ardhi.
Nitapata hati ya umiliki?+
Makazi Solutions inasaidia maandalizi na mchakato wa hati za umiliki, ikiwemo Certificate of Right of Occupancy (CRO) na Certificate of Customary Right of Occupancy (CCRO), kulingana na aina ya umiliki wa ardhi.
Je, napewa risiti ya malipo?+
Ndiyo. Kila malipo yanapaswa kuwa na risiti rasmi ya kampuni. Usilipe bila kupokea risiti.
Naweza kutembelea eneo kabla ya kununua?+
Ndiyo, na tunashauri ufanye hivyo. Panga site visit kwa kutupigia simu au kutuandikia WhatsApp 0790 398 189.
Mradi uko wapi hasa?+
Kipumbwi, Wilaya ya Pangani, Mkoa wa Tanga, kando ya Bahari ya Hindi, takribani kilomita 1.5 kutoka Bandari ya Kipumbwi.